Mbunge
wa Mtwara Mjini (CUF), Maftaha Nachuma amewataka wananchi wa jimbo hilo
kupuuza taarifa zinazosambaa kwamba ana mpango wa kujiondoa katika
chama hicho.
Amesema anaendelea kuwatetea wakazi hao ili wapate maendeleo.
“CUF
hawana historia ya kuhamahama vyama, hata huyo aliyeondoka ameondoka
kwa masilahi binafsi. Mimi Maftaha Nachuma nitakuwa wa mwisho kuondoka
CUF,” alisema jana Jumatano Desemba 6,2017.
Alisema
suala la wabunge kujitoa katika nafasi zao linasababishwa na njaa
kutokana na kuangalia masilahi binafsi bila kutetea wananchi.
Nachuma
alisema wabunge wengi walidhani wakipata nyadhifa hizo watakuwa
wananufaika kwa kupata fedha lakini sasa hilo halipo kwa kuwa ubunge
siyo dili bali ni kwa ajili ya kuwatumia wananchi.
Kupitia mitandao ya kijamii imeelezwa kwamba mbunge huyo ana mpango wa kujiondoa CUF na kujiunga na CCM.
Nachuma alisema wanaosambaza taarifa hizo wana nia mbaya ya kumchafua kwa masilahi binafsi.
0 comments:
Post a Comment