Jeshi
la Polisi limetaka liachwe liendelee kufanya kazi yake kwa weledi
katika kushughulikia suala la Mtanzania aishiye ughaibuni, Mange
Kimambi, ambaye anatuhumiwa kuchapisha taarifa zinazodaiwa kuwatusi
mitandaoni watu mbalimbali wakiwamo viongozi.
Akizungumza
na Nipashe kuhusiana na uwezekano wa wao kuifunga akaunti ya Kimambi
ikiwa sehemu ya hatua wanazochukua kwa sasa, Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Barnabas Mwakalukwa, alisema ni kweli jeshi lao linalifanyia kazi suala
hilo.
Hata
hivyo Mwakalukwa hakutaka kukubali au kukataa juu ya kile kilichodaiwa
kutokea kwenye akaunti ya Kikambi na badala yake kutaka apewe muda wa
kulifanyia kazi ndipo alitolee maelezo ya kina.
“Hili
jambo lina mambo mengi sana. Watu wengi wanahusika na taasisi nyingi
(pia) zitahusika kulishughulikia, Hivyo tunaendelea kupokea mawazo ya
watu mbalimbali kuhusu namna ya kwenda nalo… mawazo wanayotupa
tunayafanyia kazi lakini naomba mtuache kwanza tunaendelea
kulishughulikia,” alisema Mwakalukwa.
Aidha
wakati Msemaji wa Polisi akisema hayo, TCRA ilisema kuwa haiwezi
kufunga wala kuingilia akaunti ya Kimambi kwa sababu huo siyo wajibu
wake kisheria.
Msemaji
wa TCRA, Semu Mwakyanjala, aliiambia Nipashe kuwa mamlaka yao haina
nguvu za kisheria kufanya kazi hiyo bali wenye wajibu wa kufanya hivyo
ni kitengo cha kudhibiti uhalifu wa mitandaoni cha Jeshi la Polisi.
Akifafanua
zaidi, msemaji huyo alisema makosa yote yanayohusu mitandao, yakiwamo
ya watu kutishiwa maisha, kutukanwa, kuibiwa kwa njia ya mtandao au
kunyanyaswa kwa namna yoyote mtandaoni, wanaohusika ni polisi na siyo
TCRA.
“Masuala
ya akaunti za watu kwenye mitandao kama hiyo unayosema (ya Kimambi)…
mwenye mamlaka ya kuingia na kuzifunga ni Jeshi la Polisi. Bunge liliipa
mamlaka ya kisheria polisi kuchunguza na kukamata wahalifu kama hao…
waulizeni wao,” alisema Mwakyanjala.
Hata
hivyo zipo taarifa mitandaoni zilimkariri Mtanzania huyo aishiye
Marekani kuwa kilichotokea ni matokeo ya kazi ya wadukuzi wa mitandaoni,
maarufu kama ‘hackers’ kupoteza akaunti yake yenye wafuasi takribani
milioni 1.5.
Pamoja
na hayo upo ujumbe wa lugha ya kigeni uliokuwa ukisambaa kwenye mtandao
wa instagram ukionyesha kuwa akaunti inayofahamika kuwa ni ya Kimambi,
imefungwa na waendeshaji wa mtandao wa Instagram kwa sababu ya kuwapo
kwa malalamiko dhidi ya machapisho ya akaunti hiyo.
0 comments:
Post a Comment