Wednesday 6 December 2017

Uganda-Mke wa Besigye,Winnie Byanyima ateuliwa tena kuongoza Oxfam


Winnie Byanyima ameteuliwa tena kwa kipindi cha miaka mitano kuongoza kama mkurugenzi mkuu wa Oxfam.
Byanyima, amabye ni raia wa Uganda alijiunga na Oxfam mwaka 2013 na amewahi kuwa mbunge kwa miaka 11 na pia kufanya kazi katika Umoja wa mataifa.
Mwenyekiti wa Oxfam Juan Alberto Fuentes amemtaja Byanyima kama kiongozi mwenye maono na aliye msitari wa mbele kupigania usawa na kupambana na umaskini.
Oxfam ni shirika la misaada linalojihusisha sana na miradi ya kupunguza umaskini kama vile biashara ndogo ndogo na kilimo.

0 comments:

Post a Comment