Wednesday 6 December 2017

UNEP yatoa tuzo kwa walinda mazingira hodari



     
Shirika la Umoja wa mataifa la kuhifadhi mazingira UNEP limetoa tuzo sita kubwa kwa watu na mashirika yaliotoa mchango mkubwa katika uhifadhi wa mazingira.
Mojawepo wa waliopokea tuzo ni jamii ya watu wa Saihanba nchini China ambao ndani ya vizazi vitatu wamefanikiwa kupanda msitu kwenye eneo ambalo lilikuwa jangwa.
Hafla ua kutoa tuzo hizo imefanyika katika makao makuu ya shirika la UNEP mjini Nairobi ambako mkutano wa 3 wa mawaziri wa mazingira unaendelea.
Katika miaka ya 1960 eneo la Saihanba lilikuwa ni jangwa lenye vumbi, joto na hakukuwa na dalili ya maisha.
Lakini wakati huo serikali ilianza juhudi za kubadilisha jangwa kuwa msitu katika zaidi ya nusu karne iliyopita.
Juhudi zao zimezaa matunda.
Na leo shirika la Umoja wa mataifa la kuhifadhi mazingira UNEP linatoa tuzo kwao la Champion of the Earth kwa juhudi za kupanda miti na kuondoa jangwa.
Mkurungezi wa shirika hilo la UNEP bwana Erik Solheim akitoa hotuba pindi tu baada ya kukabidhi tuzo hilo anasema mfano wa Saihanba ni wa kuigwa ili kuangamiza jangwa kote duniani.
"Dunia inahitaji kupanda misitu kwa haraka, tunahitaji kuwa na kijani katika maeneo mengi na tunahitaji kurejesha misitu yetu na Saihanba inaweza kutuhamasisha sisi wote kwa sababu vizazi vitatu wamepanda miti kwenye eneo hilo na sasa tunaona jinsi msitu murejea na kuenea sana. Kwa hivyo naona ni mafanikio makubwa kwa watu Saihanba, kaskazini mwa China na sasa ni hamasisho kwa dunia nzima"
Msitu wa Saihanba una ukubwa wa hekta elfu 74.7 na ni msitu mkubwa zaidi duniani uliopandwa na watu.
Mwaka 1962, wafanyakazi 369 walianza kufanya kazi za kupanda miti kwenye shamba hilo na ndani ya vizazi vitatu
Kwa kawaida wakati wa majira ya baridi, theluji inakuwepo kwa miezi 7 kila mwaka, na wakati wa joto linafikia nyuzi 43.
Lakini safari ya kubadilisha jangwa kuwa msitu haikuwa rahisi kama anavyoeleza Chen Yanxian ambaye ni miongoni mwa kizazi cha kwanza kuanza kupanda miti Saihanba na alikuwa hapa kupokea tuzo hilo.
"Saihanba iko katika uwanda wa juu, wakati huo mazingira ya
kimaumbile ni mabaya sana na hata mazingira ya kuishi pia ni mabaya . Katika majira ya baridi , baridi inaweza kufika nyuzi 40 chini ya sufuri na katika majira ya joto ni kavu sana . Eneo kubwa ni jangwa na hakuna mti hata mmoja. Katika mazingira hayo, kutaka
kufanikiwa kupanda miti siyo jambo rahisi. Kwa kubadilisha sehemu hiyo kuwa nzuri na yenye miti mingi, kweli tulipitia shida nyingi ambazo watu hawawezi kujua. Lakini tulikuwa na imani kubwa kwamba lazima tufaulu kupanda miti katika sehemu
hiyo na kuhakikisha miti hiyo inaweza kukua na kuwa miti mikubwa."
Msitu huu sio tu umesaidia kupunguza kuenda kwa jangwa na kuvutia watalii lakini pia umekuwa na manifaa kwa mji mkuu Beijing.
Zamani upepo wenye mchanga uliingia Beijing kupitia eneo hilo, lakini sasa msitu huo umezuia vizuri mchanga wa jangwani kupeperushwa kusini.
Hali ya hewa na mazingira ya msitu wa Saihanba pia imeboreshwa, sasa aina 1,757 za wanyama na mimea inaishi katika msitu huo.
Bibi Chen Yanxian sasa anatazama mazingira ya Saihanba na macho yenye matumaini kwamba kwa kujitolea watu wanaweza kuleta mabadiliko ya kufaa kwa mazingira.
"Miaka 55 iliyopita , mimi na wenzangu kwa jumla watu 369
tulifika Saihanba wakati huo watu wengi walikuwa chini ya umri wa 24. Vizazi vitatu walifanya kazi kwa makini sana kwa kubadilisha jangwa kuwa sehemu yenye miti mingi. Tunaona fahari kujenga sehemu hiyo ambayo ni ajabu , tunaona furaha kupata tuzo hili na jambo hilo linalotatuhamasisha kuendelea kufanya kazi nzuri zaidi na kuhamasisha wachina wengi kushirki kwenye kazi hiyo na hatimaye kutokana na juhudi zetu, nyumbani kwetu lazima patakuwa pazuri zaidi."
Wengine walipokea tuzo ni pamoja na mwanzilishi wa baiskeli za Mobike kutoka China, Mamlaka ya Marekani ya Usafiri wa Anga NASA na Rais wa Chile kwa juhudi zake za kulinda bahari na kuzalisha kawi safi

0 comments:

Post a Comment