Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umemchagua Kheri James kuwa mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
James amepata kura 319 kati ya kura 583 zilizopigwa akimwacha kwa mbali mpinzani wake, Thobias Mwesiga aliyepata kura 127.
Uchaguzi huo uliofanyika Jumapili Desemba 10,2017 ukihusisha wagombea saba kwa nafasi ya mwenyekiti.
Katika
uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa UVCCM, Thabia Mwita ameshinda kwa
kupata kura 286 dhidi ya mpinzani wake Rashid Mohamed Rashid aliyepata
kura 282.
Msimamizi wa uchaguzi huo alikuwa William Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Wagombea
wengine waliochaguliwa ni mwakilishi wa vijana katika jumuiya ya Umoja
wa Wanawake (UWT), Dotto Nyirenda; mwakilishi wa vijana kwenda Jumuiya
ya Wazazi, Amir Mkalipa na wawakilishi watatu wa Tanzania Bara kwenda
Baraza Kuu la UVCCM ambao ni Rose Manumba, John Katarahiya na Secky
Kasuga.
Wengine ni wawakilishi wawili wa Zanzibar kwenda Baraza Kuu la UVCCM ambao ni Nasra Haji na Abdallah Rajabu.
Pia, wajumbe wawili kutoka Zanzibar wanaokwenda Halmashauri Kuu ya Taifa, Abdallaghari Idrisa Juma na Maryam Mohamed Khamis.
Wengine
waliochaguliwa ni wajumbe watatu kutoka Tanzania Bara wanaokwenda
Halmashauri Kuu ambao ni Sophia Kizigo, Mussa Mwakitinya na Keisha.
Akizungumza
baada ya kutangazwa mshindi, mwenyekiti James amewataka vijana kufanya
kazi kwa bidii na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na mwenyekiti wa CCM,
Rais John Magufuli.
Ameagiza
viongozi wa umoja huo hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa akifungua
mkutano wa tisa wa UVCCM ichapishwe na nakala zisambazwe kwa vijana
mikoani na wilayani ili kutekeleza maagizo aliyoyatoa ikiwamo kupambana
na rushwa na ubadhirifu wa mali za jumuiya hiyo.
0 comments:
Post a Comment