Tuesday 12 December 2017

Kampuni ya China yapanga kujenga kutoa mafunzo kwa Vijana Uganda

Vijana kadhaa wa China wanapanga kujenga Kituo cha mafunzo kwa vijana wenyeji mjini Kampala, Uganda, kwa ajili ya kuwasaidia kufanya kazi katika sekta ya mafuta na gesi.

Kituo hicho kitakachogharamia dola milioni 4.53 za kimarekani kitatoa mafunzo kwa vijana wa Uganda kufanya kazi katika uzalishaji wa mafuta. Ujenzi wake unapangwa kukamilika mwezi Februari mwaka kesho. Katika mwaka wa kwanza, kituo hicho kinatarajiwa kutoa mafunzo wa wanafunzi 1,600, na kinalenga kuongeza idadi hiyo hadi kufikia 11,000 kila mwaka katika siku zijazo.

0 comments:

Post a Comment