Benki
ya Dunia imetoa ufadhili wa shilingi Bilioni 47 kutekeleza mradi wa
uhifadhi wa rasilimali za maji awamu ya pili katika bonde la mto Wami.
Akizindua
mradi huo jana, Mjini Dodoma Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi
Isack Kamwelwe alisema kuwa Tanzania ina jumla ya mabonde tisa ya maji
lakini mabonde hayo yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za
kibinadamu na kiuchumi zinazosababisha kupungua kwa maji katika mabonde
hayo.
"Fedha
hizi zilizotolewa na Benki ya Dunia zitaenda kutoa elimu kuanzia ngazi
ya juu mpaka mwananchi wa kawaida juu ya njia za kutumika kutunza
rasimalimali za maji ndani ya hifadhi ya bonde la mto Wami," alisema
Mhandisi Kamwelwe.
Aidha
Mhandisi Kamwelwe amewataka wananchi na viongozi watakaopata elimu hiyo
kutunza rasilimali hiyo wao wenyewe kwa kutofanya shughuli za
kibinadamu na za kiuchumi ndani ya hifadhi la bonde hilo.
Kwa
upande wake, mwakilishi wa Benki ya Dunia Alex William amesema kuwa
jukumu la utunzaji wa rasilimali za maji ni za kila mwananchi, kiongozi
pamoja na taasisi za umma na binafsiHivyo amewata Watanzania kupitia
mradi huo kutunza rasilimali hiyo ili kuongeza kiwango cha maji ndani ya
bonde hilo ambayo yatatumika katika shughuli za nyumbani, viwandani,
mashambani katika shughuli za uvuvi pamoja na utalii.
Naye,
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Nazifa
Kemikimba amesema mradi huo utasaidia upatikanaji wa maji katika Jiji la
Dar es Salaam na mikoa ya karibu ukiwemo mkoa wa Morogoro.
0 comments:
Post a Comment