Tuesday 23 January 2018

Bunge la Marekani laidhinisha matumizi ya shirikisho


Bunge la Seneti nchini Marekani limeidhinisha matumizi ya muda kufadhili serikali ya shirikisho, katika kumaliza mjadala uliozua sitofahamu kwa siku tatu.
Muswada huo, ulioidhinishwa na idadi kubwa ya maseneta, utasaidia ufadhili wa huduma za shirikisho kwa wiki nyingine mbili na nusu.
Muswada huo pia umepelekwa Baraza la Wawakilishi na baadaye kusainiwa na Rais Trump.
Wawakilishi wa Democratic walisema kuwa wataunga mkono muswada huo kama utatoa hatma ya maelfu ya wahamiaji waliongia marekani wakiwa watoto ambapo sasa wanakabiliwa na kurudishwa sehemu walizotoka.
Hadi sasa wahamiaji hao wanalindwa na program ya kuwasadia watu walioingia marekani wakiwa watoto DACA.
Akizungumza baada ya kura hizo za seneti kiongozi wa Republic Mitch McConnell amezitaka pande zote mbili kuingia katika makubaliano yenye tija.

0 comments:

Post a Comment