Tuesday, 23 January 2018

Katibu mkuu wa UN aanza kufuatilia tukio la kimabavu dhidi ya waandamanaji DRC



Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric jana amesema, katibu mkuu Bw. Antonio Guterres anafuatilia sana tukio la kimabavu dhidi ya waandamanaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.


Kwenye taarifa Bw. Dujarric amsema, Bw. Guterres amevitaka vikosi vya usalama wa DRC vijizuie, na kulinda uhuru wa kutoa maoni na haki ya kuandamana kwa amani.
Taarifa inasema, jumapili polisi wa DRC walitumia nguvu wakati wa kutawanya maandamano dhidi ya rais Joseph Kabila, na kusababisha vifo vya watu 6 na wengine 63 kujeruhiwa.
Bw. Guterres ameitaka serikali ya DRC ifanye uchunguzi kuhusu tukio hilo na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.

0 comments:

Post a Comment