Saturday 20 January 2018

Mtoto mwenye ulemavu aonyesha kipaji cha hali ya juu mbele ya Diamond



Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameshangazwa na kipaji cha mtoto mwenye ulemavu wa macho huko nchini Rwanda baada ya mtoto huyo kuimba nyimbo zake mbili ile hali hata hajui lugha ya kiswahili.
Diamond akiwa na watoto wenye ulemavu wa macho mapema leo jijini Kigali, Rwanda
Diamond Platnumz ambaye yupo nchini Rwanda kwa ziara yake binafsi ameshangazwa na mtoto huyo kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa macho (Vipofu) cha Jordan Foundation huko Gatsata, Jijini Kigali.

0 comments:

Post a Comment