Shirika la Umoja wa Mataifa la
kuwahudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA limetangaza kuwa leo litazindua
kampeni ya kuchangisha fedha ili kukabiliana na pengo kubwa la bajeti
kwa ajili ya wakimbizi hao.
Mshauri wa habari wa shirika hilo Bw. Adnan Abu Hasna amesema, mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Pierre Krahenbuhl atakutana na wanahabari leo huko Gaza ambapo atazindua kampeni hiyo.
Mkutano huo utaitaka jumuiya ya kimataifa itoe msaada wa fedha kulisaidia shirika hilo liendelee na kazi ya kuwahudumia wakimbizi wa Palestina. Bw. Abu Hasna amesema shirika hilo linakabiliwa na changamoto kubwa zisizowahi kutokea.
Marekani imeamua kupunguza msaada kwa shirika hilo kutoka dola za kimarekani milioni 125 hadi dola za kimarekani milioni 65 mwaka 2018.

0 comments:
Post a Comment