Chama cha Social Democratic SPD kimepiga kura kuunga
mkono kuanza kwa mazungumzo ya mwanzo ya kuunda serikali ya
mseto na chama cha kansela Angela Merkel.
Hatua hiyo imeliingiza taifa hilo ambalo ni uchumi mkubwa
katika bara la Ulaya hatua moja karibu na kupata serikali
imara baada ya miezi kadhaa ya hali ya sintofahamu ya kisiasa.Wajumbe wa chama cha SPD walipiga kura 362 za 'ndio' dhidi ya kura 279 za 'hapana" kusongambele na majadiliano baada ya viongozi wa chama hicho cha siasa za wastani zan mrengo wa kushoto kukubali muongozo wa muungano pamoja na kundi la vyama vya kihafidhina vinavyoongowa na kansela Merkel mapema mwezi huu. Hakuna mjumbe aliyejizuwia kupiga kura.
Mazungumzo yanatarajiwa kuanza wiki hii, na kuleta ahueni kwa washirika wa Ujerumani barani Ulaya , ambako Merkel kwa muda mrefu amechukua nafasi ya uongozi katika masuala ya kiuchumi na usalama. Wajumbe wa chama cha SPD bado watakuwa na nafasi ya kupiga kura katika makubaliano ya mwisho ya kuunda serikali , kama yatapatikana.
Kiongozi wa chama cha Social Democratic SPD Martin Schultz hapo awali katika hotuba yake kwa wajumbe aliwataka wanachama wa chama hicho kupiga kura kwa ajili ya kufungua mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto na chama cha kansela Merkel, akisema serikali imara ya Ujerumani inahitajika kuimarisha Ulaya na kuwa kama ukuta dhidi ya siasa kali za mrengo wa kulia.
Uamuzi wake ulikuwa sahihi
Chama hicho cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto kimeshiriki katika serikali na kundi la vyama vya kihafidhina la kansela Angela Merkel tangu mwaka 2013, lakini Schultz aliapa kutorejea tena katika kile kinachoitwa "muungano mkuu" baada ya chama chake cha Social Democratic kupata kipigo katika uchaguzi wa mwezi Septemba.
0 comments:
Post a Comment