Serikali ya Ethiopia imesema, waasi 148 wamejisalimisha kwa vikosi vya usalama vya Ethiopia katika wiki kadhaa zilizopita. Mkuu wa jimbo la Gambella Bw. Gat Luack amesema, waasi hao waliojisalimisha wanasemekana kuwa ni wanachama kutoka kundi la waasi la GPLM.
Bw. Luack pia amesema, kabla ya hapo waasi hao walikuwepo nchi
jirani ya Eritrea, lakini wameamua kurudi Ethiopia kushiriki kwenye
shughuli za amani na maendeleo za nchi hiyo.
Serikali ya Ethiopia inashutumu kuwa kundi hilo la waasi linaungwa mkono na nchi pinzani Eritrea, wakati Eritrea ikilaumu Ethiopia kuunga mkono makundi ya waasi nchini Eritrea na kufanya kampeni ya kimataifa kuitenga nchi hiyo.

0 comments:
Post a Comment