Tuesday 27 February 2018

Rais wa Afrika Kusini alibadilisha baraza la mawaziri


Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amelifanyia mabadiliko baraza la mawaziri, na kumteua makamu mwenyekiti wa chama cha ANC, Bw. David Mabuza kuwa naibu rais wa nchi.
Mabadiliko yaliyofanywa ni pamoja na ya waziri wa fedha Bw Malusi Giaba anayekuwa waziri wa mambo ya ndani, waziri katika ofisi ya rais anayeshugulikia usimamizi na tathmini Jeff Radebe anakuwa waziri wa nishati. Waziri wa zamani wa fedha Bw Nhlanhla Nene amerudishwa tena kwenye wizara hiyo.
Rais Ramaphosa amesema, amezingatia kwa makini uwiano kati ya kudumisha utulivu, kufufua uchumi na kuharakisha mageuzi, na kwamba mabadiliko hayo yanalenga kuhakikisha kuwa serikali inaweza kutekeleza kikamilifu mamlaka iliyopewa.

0 comments:

Post a Comment