Monday 26 February 2018

Serikali ya Nigeria kuwasaka wasichana 110 waliochukuliwa na Boko Haram


Mamlaka nchini Nigeria imesema imeongeza nguvu ya ndege za kivita ili kuweza kuwasaka wanafunzi wasichana waliotekwa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Serikali inasema takriban wasichana 110 hawajulikani walipo baada ya wanamgambo wa kiislam kuwateka katika shule yao iliyopo Dapchi.
Mapema serikali ya kijiji hicho ilililaumu jeshi kwa kushindwa kuchukua hatua hata baada ya kupewa taarifa.

0 comments:

Post a Comment