Saturday 24 February 2018

Shambulizi laua watu 18 Somalia



Watu 18 wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulio la bomu lililofanywa na kikundi cha Al-Shabaab jana, Februari 23 mji mkuu wa Somalia ,Mogadishu.

Magari mawili yaliyokuwa yametegeshwa mabomu yalilipuliwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu

Bomu la kwanza lililipuka baada ya washukiwa wa kikundi cha Al-Shabaab walipokaidi kusimama katika lango la kuingilia Ikulu na walirusha risasi kwa walinzi wanaolinda lango hilo
Huku Bomu la pili lililipuka kutoka katika gari ambalo lilikuwa limeegeshwa mbele ya hoteli mbali kidogo na Ikulu ya Rais

0 comments:

Post a Comment