Thursday 8 February 2018

Tottenham yafuzu kwa raundi ya tano


Klabu ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kufuzu kwa raundi ya tano ya kombe la FA nchini Uingereza kufuatia ushindi wa magoli 2-0 iliopata jana dhidi ya Newport County katika mechi ya marudiano.
Magoli ya Tottenham yalifungwa na Eric Lamela na jingine likiwa ni la Newport kujifunga kupitia Dan Butler.
Baada ya kufanikiwa kusonga mbele, Spurs sasa itakutana na Rochdale inayoshiriki ligi daraja la kwanza jumamosi ijayo Februari 18.

0 comments:

Post a Comment