Friday 2 March 2018

Kutoka kwenye Uwaasi hadi kuwa mlezi


Mwanamke mmoja anayeitwa Mariam Ndayisenga maarufu kama Mama Zulu ambaye alikuwa mwanachama wa kikundi cha waasi, kwa sasa anafanya shughuli za kulea watoto yatima

Hatahivyo mwanamke huyo ni miongoni mwa wanawake wa kwanza kujiunga na makundi ya waasi mwishoni wa miaka ya 90
Athari za vita kwa watoto ndio zilizomuhamasisha mwanamke huyu ambaye alikuwa mpiganaji wa zamani wa kundi la Waasi la CNDD/FDD kufanya kazi ya kuwalea watoto hao yatima

Alisema ''Mimi ni mama wa kwanza kabisa kuchukua silaha na kwenda kupigania nchi yangu lakini matokeo yake sikuwa ninayategemea kwa kuwa yalileta athari kubwa sana haswa kwa watoto.''
Kituo chake kina watoto zaidi ya 70 wenye rika mbalimbali wakiwemo hata watoto wachanga.

0 comments:

Post a Comment