Thursday 29 March 2018

Murray kurudi mchezzoni baada ya kufanyiwa upasuaji

 

 

Mchezaji wa Tennis wa Uingereza, Andy Murray ametangaza kupitia mtandao wake wa kijamii kuwa anaendelea vizuri na huenda akarejea kwenye michezo ya kiushindani hivi karibuni.
Murray ambaye alifanyiwa upasuaji katika eneo la juu kabisa la mguu wake, hajashiriki mashindano yoyote tangu aondolewe kwenye michuano ya Wimbledon mwezi julai mwaka jana.
Licha ya kuonyesha picha kwenye mtandao wake wa twitter kuwa yuko fiti, kutokana na ushauri wa madaktari Murray atalazimika kusalia chini ya uangalizi kwa wiki moja zaidi mjini Nice nchini Ufaransa.

0 comments:

Post a Comment