Wednesday 28 March 2018

Serikali,Diamond wafikia muafaka



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe leo Machi 27 akiwa na Naibu wake Juliana Shonza, amekutana na msanii Diamond Platnumz kwa mazungumzo

 Wengine walioudhuria mazungumzo hayo ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mwingereza na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fisoo pamoja na meneja watatu wa Diamond, Sallam Sharaff, Hamis Taletale na Said Fella

Diamond alimuahidi Waziri kushirikiana na Naibu Shonza pamoja na Uongozi mzima wa Wizara katika kusimamia maadili ya kazi za Sanaa nchini na kuwa mfano wa wasanii wenzake


Waziri Mwakyembe alisisitiza kwamba Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo yanafanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa kiongozi au Wizara


Naye Naibu Waziri alisisitiza umuhimu wa wanasanaa kufuata taratibu na kuwasilisha kazi zao mapema katika mamlaka husika ili kuepusha matatizo baadaye

0 comments:

Post a Comment