Wednesday 28 March 2018

Marais wa China na Korea Kaskazini wakutana



Kutokana na mwaliko wa rais Xi Jinping wa China, kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un amefanya ziara isiyo rasmi nchini China na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao wawili wamebadilishana maoni kuhusu hali ya kimataifa na ya Peninsula ya Korea.
Rais Xi Jinping amesema tokea mwaka huu, hali ya Peninsula ya Korea imeonesha mwelekeo mzuri, na China inapongeza juhudi zilizofanywa na Korea Kaskazini. Amesisitiza kuwa China siku zote inashikilia lengo la kuifanya peninsula hiyo iwe sehemu isiyo na silaha za nyuklia, kulinda amani na utulivu katika peninsula hiyo, na kutatua masuala kwa njia ya mazungumzo.
Kwa upande wake Bw Kim Jong-un amesema Korea Kaskazini imedhamiria kubadilisha uhusiano kati yake na Korea Kusini kuwa uhusiano wa ushirikiano na maafikiano, kuwa na mazungumzo kati ya viongozi wa pande hizo mbili, na pia inapenda kufanya mazungumzo na Marekani. Amesema katika mchakato huo, Korea Kaskazini pia inatumai kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na China, ili kulinda kwa pamoja amani na utulivu katika peninsula hiyo.

0 comments:

Post a Comment