Wednesday 28 March 2018

Wanafunzi watano wa kiume wakamatwa katika shule ya wasichana



Wanafunzi watano wa kiume wakamatwa nchini Kenya wakiwa wamevaa mavazi ya wanafunzi wa kike huku wakijaribu kuingia katika vyoo vya shule ya wasichana. .

 Wanafunzi hao kutoka shule ya sekondari St Mary's Kibabii Boys walitiwa nguvuni baada ya kukutwa wakiwa katika mavazi ya kike katika shule ya jirani ya wasichana ya Cardinal Otunga Girls' High School .

Kwa mujibu wa mwalimu wa zamu katika shule ya wasichana Cardinal Otunga amesema kuwa majira ya saa kumi na moja walihisi kishindo karibu na ukuta wa choo ndipo katika harakati za kufatilia waliwakuta wamejificha chooni huku wakiwa wamevalia mavazi ya kike.

0 comments:

Post a Comment