Wednesday 28 March 2018

NATO Kutimua wajumbe 7 wa Russia


Katibu mkuu wa Shirika la kujihami la nchi za magharibi NATO Bw. Jens Stoltenberg ametangaza kuwa NATO litabatilisha vitambulisho vya wajumbe 7 wa kudumu wa Russia kwenye makao makuu ya NATO.
Bw. Stoltengerg amesema tangu tarehe 4 Machi jasusi wa zamani wa Russia alipowekewa sumu nchini Uingereza, nchi wanachama wa NATO zilifanya majadiliano na kuamua kuchukua hatua za pamoja zenye nguvu, hadi sasa nchi 25 wanachama na nchi washirika wa NATO zimewafukuza wanadiplomasia zaidi 140 wa Russia.
Habari nyingine zinasema kuwa rais Donald Trump wa Marekani tarehe 27 kwa nyakati tofauti alizungumza kwa njia ya simu na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel, na kujadiliana nao kuhusu kuwafukuza wanadiplomasia wa Russia na masuala ya biashara kati ya Marekani na Ulaya. Ikulu ya Marekani siku hiyo ilitoa taarifa ikisema rais Trump na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wanaunga mkono kuwafukuza wanadiplomasia wa Russia, kujibu tukio la kuwekewa sumu kwa aliyekuwa jasusi wa Russia.

0 comments:

Post a Comment