Wawakilishi kutoka serikali za
nchi za Afrika, sekta binafsi, taasisi za fedha na utafiti wanapanga
kukutana nchini Kenya kujadili ushirikiano na usafirishaji wa
teknolojia, ili kusaidia kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali
ya hewa.
Bw. Jukka Uosukianen ambaye ni mkurugenzi wa kituo na mtandao wa teknolojia ya hali ya hewa cha Umoja wa Mataifa kinachoandaa mkutano huo, amesema mkutano huo unafanyika wakati Afrika inakabiliana na changamoto kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa, ongezeko la ukame, mvua kubwa na mafuriko, ambazo zina athari kwenye usalama wa chakula.
Bw Uosukianen amesema kituo chake kinahimiza maendeleo na usafirishaji wa teknolojia zisizosababisha uchafuzi, na kuzisaidia nchi zinazoendelea kupata teknolojia.
Amesema kwa sasa teknolojia zaidi ya 100 ziko njiani kwenda kwenye nchi zaidi ya 75 duniani, zikiwa ni za sekta za kilimo, nishati, viwanda na usafirishaji.

0 comments:
Post a Comment