Sunday 15 April 2018

Fatma Karume ashinda urais TLS


Wakili msomi Fatma Amani Karume amechaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika(TLS) akichukua kijiti kutoka kwa Wakili Tundu Lissu

Wakili Fatuma amechaguliwa kwa kura 820, akiwashinda Mawakili wengine watatu ambao ni, Wakili Simba Ngwilimi(Kura 363), Wakili Musa Mwapongo(Kura 12) na Wakili Godfrey Wasonga(Kura 6)

Ushindi huu unamfanya Fatma kuwa mwanamke wa pili kushika nafasi hiyo toka kuanzishwa kwa TLS(1954). Mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo alikuwa Jaji Joaquine De Mello

0 comments:

Post a Comment