Thursday 19 April 2018

Jeshi la Iraq lapambana na IS,laua magaidi 4


Jeshi la serikali ya Iraq limewaua wapiganaji wanne wa kundi la Islamic State kwenye operesheni ya msako dhidi ya wapiganaji waliosalia wa kundi hilo iliyofanyika jana katika mkoa wa Salahudin, ulioko katikati mwa Iraq. Polisi mkoani Salahudin wamesema jeshi la serikali lilitumia helikopta za kivita na mizinga kufanya mashambulizi dhidi ya maficho ya wapiganaji wa IS kwenye maeneo ya milimani, wapiganaji wanne wa IS na askari mmoja wa jeshi la Iraq waliuawa kwenye operesheni hiyo.

0 comments:

Post a Comment