Thursday 19 April 2018

Saudi Arabia yaungana na Marekani nchini Syria



Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir amesema, nchi hiyo inashauriana na Marekani kuhusu kutuma jeshi nchini Syria.
Bw. Al-Jubeir amesema hayo alipokutana na waandishi wa habari akiongozana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guerres ambaye yupo ziarani nchini humo. Bw. Jubeir amesema, tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Saudi Arabia inashauriana na Marekani kuhusu kutuma jeshi nchini Syria kuchukua nafasi ya jeshi la Marekani pale. Hivi sasa, pande hizo mbili zinajadiliana kuhusu ukubwa wa jeshi la Saudi Arabia litakalotumwa mashariki mwa Syria.
Habari zinasema, hivi sasa, wanajeshi wapatao elfu 2 wa Marekani wako nchini Syria ambao wanasaidia kikosi cha Kikurd kupambana na kundi la IS nchini humo.

0 comments:

Post a Comment