Thursday 12 April 2018

Wanamichezo 8 wa Cameroon 'waingia mitini' Australia.


Wanamichezo 8 kutoka Cameroon wametoweka katika makazi yao waliyofikia katika michezo ya jumuiya ya madola nchini Australia. Kocha wa timu hiyo Simon Malombe ameongea na BBC katika press na kuthibitisha kutoweka kwa wanamichezo hao na wametoa taarifa polisi tayari wafanye uchunguzi walipoenda.

 
Wanamichezo watatu kati ya 8 waliopotea mara ya mwisho walionekana jumatatu na jumanne katika mida tofauti na maeneo tofauti. Wanamichezo hao kutoka Cameroon visa zao za kuishi nchini Australia zitaisha tarehe 15 May.


Waliopotea ni wabeba vitu vizito Matam Matam, Arcangeline Fouodji Sonkbou, Petit Minkoumba pamoja na mabondia Christian Ndzie Tsoye, Simplice Fotsala, Arsene Fokou, Ulrich Yombo na Christelle Ndiang.


Hii sio mara ya kwanza mwaka 2012 wanamichezo saba 7 wa Cameroon waliopotea London, Uingeleza katika michezo ya Olympics.

0 comments:

Post a Comment