Thursday 12 April 2018

Mama mbaroni kwa kumpikia mtoto bangi-Marekani



Jijini Arizona, Alaina Marie anashikiriwa na polisi baada ya mtoto wake kula bangi iliyochanganywa kwenye makaroni na mkate na kumfanya mtoto wake alewe. Alaine alimpa chakula mwanae wa miaka miwili chakula ambacho alipika kwa ajiri ya mume wake na hakujua kwamba kitaleta madhara kwa mtoto.
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Baada ya mtoto kuanza kubadilika walimpeleka hospital na ndipo kubainika mtoto alikula bangi na madaktari ndio walitoa taarifa polisi. Police baada ya kupata taarifa walifika hadi nyumbani kwa Alaine na kukuta watoto wadogo wengine watatu na kuwachukua kuwakabidhi idara ya watoto ya Arizona.

Polisi walifanya upekuzi ndani ya nyumba na kufanikiwa kukuta miti miwili ya bangi imepandwa ndani ya garage ya nyumba hiyo pamoja na vyakula vilivyopikwa kwa bangi ndani ya friji.

Alaine amefunguliwa shitaka la child abuse na anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 19 April.

0 comments:

Post a Comment