Sunday 6 May 2018

Askofu Malasusa apata watetezi



Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya Kanisa Kuu la Kilutheri Tanzania (KKKT), imesema bado inamtambua Baba Askofu Dkt. Alex G. Malasusa kama Askofu wa Dayosisi hiyo na itaendelea kushikamana naye katika kuiongoza na kuihubiri Injili ya Yesu Kristo

Kupitia kikao cha Halmashauri Kuu, Dayosisi hiyo ilijadili na kujiridhisha kuhusu barua aliyoandikiwa Askofu Malasusa kwamba alikiuka mapatano ya Mkutano wa Maaskofu wa KKKT

Dayosisi hiyo imesema haina lengo la kupingana na Maazimio ya Mkutano wa Maaskofu na maelekezo yote yaliyotolewa na KKKT Makao Makuu yamezingatiwa.

Aidha, Halmashauri Kuu imewataka washirika wake wawe watulivu wakati ikiendelea kulifuatilia jambo hili kwa makini.

0 comments:

Post a Comment