Sunday 27 May 2018

Cover ya Albamu ya Pusha T yaichukiza familia ya Whitney Houston


Familia ya Whitney Houston haijafurahia cover ya album mpya ya Pusha T “Daytona” wamedai kuwa imewarudishia maumivu

Damon Elliott, mmoja wa ndugu wa Whitney ameongea na jarida la “People” amesema aliiona hiyo cover kupitia kwa binti yake mdogo, amedai kuwa hawakutegema kama Kanye West anaweza kutumia maumivu ya watu wengine ili kujinufaisha mwenyewe kwa kupata kiki na mauzo ya album

Damon amemtaka Kanye West aiombe msamaha familia ya Whitney Houston na kuibadilisha hiyo cover haraka sana

Pusha T muda mfupi baada ya kuonesha cover ya album yake, alisema Kanye West ndio aliipendekeza na ndio aliyotoa mkwanja wa kulipia haki za kuitumia, amedai kuwa alilipa zaidi ya Million 193 Tsh.

0 comments:

Post a Comment