Mwigizaji maarufu Elizabeth Michael amebadilishiwa kifungo na sasa ataanza kutumikia dhabu yake akiwa uraini.
Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mwanzoni mwa mwezi Novemba 13 mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba mwaka 2012.
Kwa mujibu wa MCL(Mwananchi), Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment