Thursday 15 March 2018

Rais wa Ufilipino ajinusuru na ICC



Rais Rodrigo Duterte amesema nchi yake imejitoa katika mkataba wa Roma, unaounda Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Duterte amedai ICC inatumika kama chombo cha kisiasa baada ya kuanza kuichunga nchi hiyo juu ya mauaji yanayofanywa kutokana na kampeni yake ya kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Polisi wanasema kuwa wamewaua washukiwa karibu 4,000 wa madawa ya kulevya kama sehemu ya kampeni hiyo, huku mashirika ya haki za binaadamu yakidai kuwa idadi halisi ni karibu mara tatu zaidi ya takwimu zinazotolewa na serikali.

Mahakama ya ICC ilifunguliwa mwaka 2002, ndio mahakama pekee ya kudumu ya makosa ya uhalifu ya kivita, na hushughulikia makosa makubwa kabisa ya uhalifu ambayo mahakama za kitaifa hazitaki au hazina uwezo wa kuyashughulikia

0 comments:

Post a Comment