Monday, 14 May 2018

Celtics yaitoa jasho Cavaliers kwenye mechi ya kwanza fainali za 'Eastern Conference'


Mechi ya kwanza ya fainali ngazi ya kanda ya mashariki (Eastern Conference) kwenye ligi ya kikapu ya nchini Marekani imepigwa alfajiri ya leo kwa saa za Afrika mashariki ambapo kumeshuhudiwa, mabingwa watetezi Cleveland Cavaliers ikifungwa na wapinzani wao Bolton Celtics kwa alama 108-83.
Katika mchezo huo ambao ni wa kwanza kati ya saba, kumeshuhudiwa mchezaji bora mara nne wa ligi hiyo Lebron James akifunga alama 15 ambazo ni chache zaidi katika rekodi binafsi.
Timu hizo, zitakutana tena alfajiri ya jumatano kwenye mechi ya pili.

0 comments:

Post a Comment