Wednesday 27 June 2018

Argentina yaikwatua Nigeria,yafuzu hatua ya 16 Bora


Licha ya changamoto iliyokuwepo, timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya mashindano ya kombe la dunia baada ya kupata ushindi wa lazima na muhimu wa magoli 2-1 ilipocheza dhidi ya Nigeria jana.
Katika hatua ya 16 bora Argentina sasa itakutana na Ufaransa ambayo Juni 30, na mshindi kati ya timu hizo mbili atafuzu robo fainali.
Mechi za mwisho za hatua ya makundi zinaendelea leo kwa timu kutoka makundi E na F, lakini changamoto kubwa ikiwa ni kwa baadhi ya timu, ambapo katika kundi E Serbia italazimika kushinda dhidi ya Brazil ili kufuzu, kwani sare haitawasaidia licha ya kuwa watapata alama nne ambazo zitakuwa sawa na Uswisi kama ikifungwa na Costa Rica.
Lakini kwenye kundi F, Mexico ndiyo timu pekee iliyofuzu, lakini Korea Kusini haina nafasi kabisa, hivyo kazi imebaki kwa Ujerumani na Sweden ambazo kila mmoja ina nafasi ya kufuzu.

0 comments:

Post a Comment