Wednesday 27 June 2018

Maradona augua kwa ushindi wa Argentina



Mtu mwenye heshima kubwa kwenye soka la Argentina Diego Maradona jana alilazimika kukimbizwa hospitali kwa kilichodaiwa kuwa alipata presha iliyotokana na mshtuko baada ya Argentina kupata goli la pili na la ushindi mechi dhidi ya Nigeria.
Katika mechi hiyo iliyochezwa mjini St. Petersburg, hadi kufikia dakika ya 85 matokeo yalikuwa 1-1 na yalikuwa si mazuri kwa Argentina kufuzu hatua ya 16 bora, jambo hilo linadaiwa kumfanya Maradona ajawe wasiwasi.
Furaha ya gafla aliyopata baada ya Argentina kupata goli la pili, ilimfanya Maradona kushindwa kutembea na alionekana kupewa huduma ya kwanza na baadae kukimbizwa hospitali, bado haijawekwa wazi tatizo lake lakini inahisiwa kuwa ni presha iliyotokana na mchezo huo.

0 comments:

Post a Comment