Nicki Minaj ame’cover jarida la “Elle” na ameongelea mambo kibao ikiwemo Kifungo cha Meek Mill na kuwa single kwa mara ya kwanza tangu akiwa na umri wa miaka 15 na album yake mpya ya “Queen”
Nicki alifunguka kuwa baada ya kuachana na Meek Mill ilikuwa mara yake ya kwanza kuwa single tangu akiwa na umri wa miaka 15, amesema ilimpa nguvu sana, anasema kwa mara ya kwanza alijisikia kama anaweza kufanya kitu chochote bila kumtegemea mtu yoyote, anasema ilimfanya ajisikie mtu mwenye nguvu
Pia alizungumzia kifungo na kesi ya Meek, amesema hawezi kumuombea mtu yoyote apitie mambo aliyoyapitia Meek
Pia ameelezea kuhusu album yake mpya ya “Queen” amesema alikuwa anatumia hadi masaa 30-36 wakati anaiandaa
0 comments:
Post a Comment