Kijana mmoja achapwa viboko 80 kwa kosa la kunywa pombe alilotenda akiwa na miaka 14
Aidha kijana huyo alitenda kosa hilo miaka 10 iliyopita na mpaka sasa haieleweki ni kwanini adhabu yake ilichelewa kutekelezwa
Shirika la Kimataifa la Amnesty limelaani adhabu hiyo iliyotekelezwa kwenye Mji ulio Mashariki mwa Jimbo la Kashmir
Ikumbukwe kuwa mwaka 2014, watu 6 walihukumiwa kwenda jela na viboko 91 baada ya kukutwa wakiuchezea wimbo wa Pharrel Williams.
Aidha, mambo mengine yanayoweza kusababisha uchapwe viboko nchini Iran ni pamoja na uzinzi, kubusu hadharani, wizi, vitendo vinavyohusiana na mapenzi ya jinsia moja.
0 comments:
Post a Comment