Bondia Anthony Joshua ameeleza
kukasirishwa na mambondia wanaopenda kubeza kila anachofanya ulingoni,
na kwamba ameendelea kunyamaza ili kuwastahi licha ya kuwa bado wanazidi
kumwandama.
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya mkutano wa kwanza na mpinzani wake katika pambano la Septemba 22, Joshua alisisitiza kuwa, yuko tayari kupigana na mwanamasumbwi yeyote ili kutetea ubingwa wake anaoushikilia kwa sasa.
Septemba 22, katika uwanja wa Wembley mjini London Joshua mwenye mikanda ya ubingwa wa dunia katika uzani mzito wa IBF, WBA na WBO anatarajiwa kupanda ulingoni kupigana na Jarrell Miller kutoka Marekani.

0 comments:
Post a Comment