Moja kati ya legend female rapper Miss Elliott atapokea Tuzo ya heshima "Lifetime Achievement Award" ama Video Vanguard Award, August 20 mwaka huu kwenye Tuzo za MTV Video Music Awards. Hii ni kwa ajili ya ubunifu wa hali ya juu kwenye video zake.
Baadhi ya video zake zilizowahi kusumbua dunia ya Hip Hop ni pamoja na: Work It, The Rain (Super Dupa Fly), Get Your Freak On, One Minute Man na Beep Me 911 ya mwaka 1997.
Wasanii wengine waliowahi kupewa Tuzo hiyo ni pamoja na Beyonce, David Bowie, Justin Timberlake, Hype Williams, LL Cool J, Janet Jackson, Kanye West pia Rihanna ambaye aliichukua mwaka 2016 na wengine wengi.
Tuzo hiyo ambayo ilibadilishwa jina mwaka 1991 na kuitwa 'Michael Jackson Video Vanguard Award' hutolewa kwa wasanii na waongozaji waliochangia na kuweka ubunifu kwenye video mbali mbali.
0 comments:
Post a Comment