Thursday 12 July 2018

Uingereza 'Yachabangwa' 2-0 na Croatia



Siku ya Jana nchini Uingereza katika mjii mkuu wa England ndege zilipita huku zikijinadi na herufi zinazosomeka "Its Coming Home" wakimaanisha kuwa kombe la Dunia ni lao bila shaka.

Lakini dakika ya 5 ya mchezo kati ya England na Croatia, Mshambuliaji Kieran Tripieer kutoka England aliipatia timu yake bao la kwanza ambalo lilidumu kwa dakika Arobaini na tano za mwanzo.

Ujumbe wa " Its Coming Home " ukaanza kufifia pale Ivan Perisic mchezaji kutoka Croatia kupachika bao la kwanza kwa timu yake katika dakika 68' na kufanya mchezo huo kuwa 1-1.

Refa Raia wa Uturuki Cuneyt Cayir akaongeza dakika 5 ambazo ndizo zikageuka mwiba kwa Uingereza ambapo dakika ya 109 Mario Mandzukic akaipatia Croatia bao la ushindi linalowapa nafasi ya kucheza fainali na Ufaransa Siku ya jumapili.

0 comments:

Post a Comment