Wednesday 15 August 2018

Russell West afanya ziara China

  •  
    Kutana na NBA Fashionista Russell Westbrook @russwest44 mshindi wa tuzo ya NBA 2018 katika kipengele cha kutokelezea (Best Stylist).

    Kwasasa mchezaji huyu wa Kikapu anayechezea Oklahoma City Thunders (OKC) ameanzisha ziara yake iitwayo "WhyNotTour"katika kulizunguka bara la Asia akianzia nchini China kwa lengo la kuwafundisha vijana mbalimbali kikapu na kutambulisha mavazi yake pamoja na viatu vyake kwa udhamini wa kampuni ya Jordan.

    Katika msimu wa Kikapu NBA 2016-2017 alikuwa akitambulika zaidi kama Mr Triple Double ni kutokana na umahiri wake wa kutupia vikapu.

    Hapa nchini Tanzania kuna wachezaji wa Kikapu wanaochezea nchi za nje kama @alphak_ na @hasheemthedream huku alpha ambaye ana kampeni yake ya Shoes For Tanzania na Hasheem ambaye huwa kwa kipindi kirefu akiwa nchini hutoa mafunzo kwa vijana mbalimbali has a katika Kikapu.

0 comments:

Post a Comment