Monday 17 September 2018

Nandy atangaza kuacha mziki ikifika 2020.


The African Prince Nandy amesema kuwa ikifika 2020 ataachana rasmi na mziki na kuanza kufanya biashara kwani ndio ndoto yake toka zamani.
.
.
Akihojiwa katika kipindi cha Leo Tena Nandy ameeleza kuwa aliweka malengo baada ya miaka kadhaa aweze kuachana na kazi ya muziki.
.
.
"Mimi ndoto zangu ni kuwa mfanyabiashara mkubwa sana na hata wakati naanza kufanya muziki nilijiwekea malengo baada ya miaka mitano niache muziki na niendeleze biashara zangu na mpaka sasa nimeitumia miaka miwili (2016 na 2017) na mwaka 2020 ndiyo nitaacha muziki, Na sio kwamba nitakuwa sitoi ngoma hapana nitakuwa natoa sema kwa mwaka hata mara moja ha show naweza kuwa nafanya mara moja kwa mwaka ili nipate muda mzuri wa kusimamia biashara zangu" @officialnandy .
.

0 comments:

Post a Comment