Wednesday, 4 April 2018
Tuesday, 3 April 2018
Takriban watu 18 nchini Nigeria wameuawa na wengine 86 kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na waasi wa Boko Haram
Waasi hao waliokuwa wakipambana na wanajeshi wa Serikali karibu na kaskazini mashariki mwa Maiduguri usiku wa kuamkia leo
Watu waliouawa wanatoka katika vijiji viwili vya Bale Shuwa na Bale Kura vilivyoko Maiduguri
Maiduguri mji mkuu wa jimbo la Borno ndiyo chimbuko la kundi hilo la waasi la Boko Haram lililoanza uasi miaka 9 iliyopita kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi na mke wa zamani wa hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini, Winnie Mandela afariki dunia mapema leo jijini Johannesburg.
Taarifa hizi zimethibitishwa na msaidizi wake, Zodwa Zwane.
Winnie atakumbukwa kwa kushiriki harakati za kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Monday, 2 April 2018
Hayo yamekuja baada tu ya mwingereza Anthony Joshua AJ kushinda na kutwaa taji kubwa la ubingwa wa masumbwi la WBO wikendi hii alipomtwanga Joseph Parker, wachambuzi wachambuzi wa mchezo huo wameanza rasmi kusubiri tangazo la kuanza kwa mchakato wa safari yake ya kuwania mkanda mwingine wa WBC unaoshikiliwa na Wilder Deontay wa Marekani.
Wilder amekaririwa akisema Joshua anapata ushindi kutokana na
upendeleo na hata hivyo hajawahi kushinda akiwa nje ya Uingereza, sasa
amewataka mapromota kuzingatia hilo.
Kwa upande wake AJ ametangaza kuwa hana tatizo na jambo hilo na yuko tayari kutoka na kwenda kupigana nje ya Uingereza na hasa kuwania huo mkanda wa WBC.
Joshua mwenye miaka 28, ni bingwa wa uzito wa juu mwenye mikanda mitatu ya WBO, IBF na WBA na hajawahi kupoteza hata pambano moja kati ya 21 aliyowahi kupigana na 20 ikiwa ni kwa Knock-Out.

Ni mara ya kwanza katika
kipindi cha miaka 28, Tottenham Spurs wamepata ushindi katika uwanja wa
Stanford Bridge katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Chelsea iliyopigwa
jana.
Licha ya Chelsea kutangulia kwa goli lililofungwa na Alvaro Morata, Spurs walisawazisha kupitia Christian Eriksen, na baadaye Delle Ali akifunga magoli mawili ya ushindi yaliyofanya matokeo ya jumla kuwa 3-1.
Kwa matokeo haya, yanafuta matumaini ya Chelsea ya kuingia nne bora kwenye msimamo wa ligi kuu kwani wanasalia na pointi 56 zikiwa zimebaki mechi chache ligi kumalizika.
Kwenye mechi nyingine zilizopigwa jana, Arsenal ilipata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Stoke City.

Rais wa klabu ya PAOK Salonika
inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ugiriki Ivan Savvidis amepewa adhabu ya
kutoingia kwenye viwanja vya mpira kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana
na kosa la kuingia uwanjani na bastola.
Machi 11, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni hasira baada ya mwamuzi kukataa goli la timu yake kwenye mechi dhidi ya AEK Athens, Saviddis aliingia uwanjani pamoja na mashabiki wengine jambo lililozusha vurugu kubwa na kupelekea serikali kusimamisha ligi kwa muda.
Kutokana na tukio hilo, timu yake ilipokwa pointi 3, imepigwa faini ya Yuro 63,000 na adhabu ya kucheza mechi tatu za ligi bila mashabiki, na Savvidis mwenyewe akipigwa faini ya Yuro 100,000.
Ligi ya Ugiriki inatarajiwa kurejea mwishoni mwa juma hili baada ya Chama cha soka cha nchi hiyo kujadiliana na Serikali juu ya usalama viwanjani.

Sunday, 1 April 2018
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amejibu Waraka wa Pasaka kutoka kwa Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ulioeleza kuhusu matukio ya kupotezwa kwa watu na kubanwa kwa demokrasia nchini
Katika ujumbe wake, Prof. Kitila amesema ni hatari kwa Kanisa kutoa kauli inayosababisha maumivu na mifarakano katika nchi badala ya kuponya
Prof. Kitila ambaye ni muumini wa KKKT, amesema anakubaliana na mengi maaskofu waliyogusia katika Waraka huo. Hata hivyo, amelitahadharisha kanisa kujiepusha na kuonekana lipo upande fulani katika mijadala ya kitaifa hususan ile inayoigusa jamii moja kwa moja
Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa kanisa kupima kwa umakini mkubwa uzito wa kila neno kabla ya kutoa kauli kwa umma.
Waraka wa Maaskofu 27 wa KKKT ulitoka hivi karibuni na kusomwa katika Makanisa yote ya Kilutheri Machi 25, 2018 ambapo kupitia waraka huo walizungumzia masuala ya Uchumi, Katiba Mpya, Siasa na Jamii kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amefafanua uwezekano wa kisayansi kwa mwanamke mmoja kubeba ujauzito mapacha kutoka kwa wanaume wawili tofauti
Amesema jambo hilo hutokea pale mwanamke anapotoa mayai mawili tofauti katika mzunguko mmoja ambayo yanaweza kurutubishwa (fertilized) na mbegu za wanaume 2 tofauti. Kisayansi inaitwa Super-fecundation.
Ndugulile ambaye ni daktari kitaaluma, ametoa ufafanuzi huo kutokana na habari kuhusu mwanamke mmoja nchini Uganda kuingia kwenye mgogoro wa kindoa na mumewe, baada ya wanaume wawili (mumewe na mdogo wake) kujikuta wote wawili ni baba wazazi halali wa watoto wawili mapacha, kila mmoja akiwa na mtoto mmoja baada ya kupimwa DNA.
"Kisayansi inawezekana. Inatokea pale mwanamke anatoa mayai mawili tofauti katika mzunguko huo mmoja ambayo yanakuwa-fertilized na mbegu za wanaume wawili tofauti. Kisayansi inaitwa superfecundation" ameeleza Dkt. Ndugulile kupitia ukurasa wake wa Twitter.