Saturday 28 October 2017

TUJIKUMBUSHE JUU YA HISTORIA YA MWANAHARAKATI MARTIN LUTHER KING JR.


Martin Luther King Jr ni moja ya wanaharakati  wakubwa sana nchini Marekani hasa ktk kupigania  haki za waamerika Weusi   ktk karne ya 20.

Alizaliwa Januari 15,1929 huko Atlanta ,Georgia nchini Marekani .Wazazi wake walimlea ktk maadili ya Dini ya kikristo na inasemekana walikuwa  viongozi wa Dhehebu la Baptist.

Nje ya kuwa mwanaharakati wa masuala ya Haki na Usawa kwa wamarekani  weusi Luther alikuwa ni Mhubiri wa Dhehebu la Baptist.

Kwa hiyo kuwa mwanaharakati wa haki za Binadamu na kuwa mhubiri ni jambo la kawaida na Mwenyezi Mungu hakatazi popote pale ktk maandiko yake matakatifu ,kwanza Mungu mwenyewe anapenda haki anachukia dhuluma,manyanyaso,Ubaguzi wa namna yeyote ile na yeye ndiye mwanzilishi na Msingi wa haki chamsingi harakati zako zisivuke mipaka ya neno lake na Taratibu za nchi yako husika.

Alijibebea umaarufu mkubwa sana kwenye Hotuba nzito sana inayojulikana kama "I HAVE A DREAM" Aliyoitoa  Agosti 28,1963 mjini Newyork  ktk Mnara wa Kumbukumbu wa Rais Abraham Lincoln  .Katika hotuba hiyo alielezea  matumaini Makubwa kwa watu weusi akisema ipo siku wamarekani weusi wataupata Uhuru na Usawa ktk Ardhi ya Amerika.

Katika hotuba hiyo watu takribani 200000 walihudhuria kumsikiliza mwanaharakati huyu wa kupinga ubaguzi ktk Amerika na Duniani kote. Aliuchukia ubaguzi wa Kirangi,Kidini,Kipato n.k .

Wakati wa karne ya 20 huko Marekani kuliibuka ubaguzi mkubwa wa Kirangi kwenye Taasisi za Kielimu ,kiafya na kidini ,vyombo vya usafiri ,Kwenye kumbi za Starehe ,Kwenye Ofisi za Umma ,Kwenye mashamba,Kwenye Viwanda ,Kwenye maduka,Kwenye masoko,n.k waamerika weusi walinyanyapaliwa sana .

Ilikuwa ukimuona mzungu  na umekaa kwenye seat unampisha ikiwa gari limejaa,ukigoma unaadhibiwa vibaya sana,mwaafrika ulikuwa huruhusiwi kula hoteli moja na mzungu ,Mwafrika hakuruhusiwa kusoma Shule  na Mzungu au mtoto wa kizungu ,Ilikuwa hairuhusiwi mzungu na mwafrika kuoana  na lilikuwa ni kosa kubwa sana kufanya hivyo n.k .Hivyo kulikuwa na hotel,hospitali ,maeneo ya burudani ,makanisa n.k ya wazungu na waafrika .

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya akina Marcus Garvey ,William Dubois ,Malcolm X walisimama kidete kutoa hotuba za kulaani vikali vitendo vibaya vya kibaguzi vilivyokuwa vinafanywa na wazungu kwa kutumia majarida,vitabu ,kuandika mapendekezo ya sheria zinazolinda watu weusi dhidi ya wazungu katika Bunge la Marekani ,walitumia Redio na Televisheni kupinga ubaguzi wa Rangi,walitumia mbinu ya maandamano kuamusha hisia za Tabaka baguliwa (Waamerika weusi) n.k .Watu hawa walifanya kazi kubwa sana ya kupinga ubaguzi uliofanywa na wazungu.

William Dubous  na wanaharakati wengine walianzisha mpango uliojulikana kama  "BACK MOVEMENT " Ukimaanisha kuwa sasa waafrika warudi kwao wakaijenge  Afrika yao ,wengi walirudi na wengine wengi pia walibaki wakiamini kuwa ipo siku wangepata Uhuru na Usawa katika Ardhi ya Amerika.William Dubous  alionyesha mfano kwa kuhama Marekani na kuja kuishi Afrika ktk nchi ya Ghana mjini Accra.

Martin Luther King Jr ni moja ya watu walioamini kuwa ukombozi utapatikana huko huko Marekani na hakuamini katika kuikimbia Marekani .Funzo tunalopata haki haipiganiwi ukiwa ng'ambo Bali ukiwa ktk nchi yako.Waswahili wanasema fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

Luther aliendelea kuwapigania waafrika huko huko Marekani na kujitwalia Tuzo kadhaa za Amani (Nobel Prizes) baada ya kuutsmbua mchango wake ktk kuwapigania waamerika weusi .

Harakati za  kupigania  Uhuru na Usawa kwa wamarekani weusi zilikuwa ngumu sana kwani kulikuwa na kikundi cha Siri kilichojulikana kama Ku Klux Klan  au Kuklux Clan kilichoundwa na wazungu ili kufifisha harakati za wamarekani weusi kudai Uhuru na usawa huko Marekani. Kikundi hiki kilikuwa hatari sana kwani kilikuwa kinawalenga viongozi wa harakati ili kiwaue .

Martin Luther king Jr aliuwa kwa kupigwa  Risasi Hapo Aprili 3,1968. Kijana  aliyetekeleza unyama huu alikuwa ni wa kizungu alijulikana kwa jina la James Earl Ray huko mjini Memphis, jimbo la Tennessee.

Martin Luther king Jr atakumbukwa kwa mbinu zake za kudai haki ,Uhuru na Usawa miongoni mwa wazungu na watu wa jamii ya kiafrika .Alidai haki ,Uhuru na usawa bila kuofia kulipa damu yake ktk harakati  za ukombozi .

Martin Luther king Jr alituma ujumbe mzito Barani Afrika,Amerika ya kusini na Asia kuwa Uhuru ,Haki na Usawa unapaswa  kuheshimiwa kwa Binadamu wote bila kujali  wewe ni wa Rangi gani ,kipato gani,Dini gani ,n.k

Martin Luther king Jr atakumbukwa sana hasa ktk hotuba yake maarufu ya "I HAVE A DREAM" Akimaanisha "Nina ndoto" ambayo ilitoa unabii mkubwa sana wa Uhuru, haki na Usawa na hatimaye Dunia ilishuhudia Marekani ikiongozwa na mwamerika mweusi mh.Barack Obama wakati miaka ya nyuma ilikuwa ni marufuku kwa wamarekani weusi kushiriki  ktk medani za kisiasa na hata kupiga kura hawakuruhusiwa .
Harakati za Martine Luther  umeleta mafanikio makubwa ndani ya
Amerika ya Leo. Kuna tofauti sana na Amerika ya Jana hasa katika kuutazama usawa  kati ya Marekani mweusi na mmarekani mweupe. Hivyo  kupitia  history hii niwaambie wanaharakati wetu kuwa kuna siku matunda ya kazi yao yataonekana

0 comments:

Post a Comment