Abiria
wa daladala inayofanya safari kati ya Gongo la Mboto na Makumbusho
jijini Dar es Salaam, jana walijikuta katika msukosuko mkubwa baada ya basi hilo
kuzimika ghafla katikati ya reli.
Ambapo tukio hilo lilisababisha abiria hao kuruka kupitia madirishani ili kujinusuru huku treni ikiwakaribia.
Tukio
hilo lilitokea jana majira ya asubuhi, eneo la kituo maarufu kama
Bakhresa, Buguruni, barabara ya Mandela na kuwafanya abiria kusukumana
na baadhi wakigombea kupita katika mlango.
Chanzo
cha kuaminika kilisema kuwa daladala hiyo yenye namba za usajili T 499
BGU na ubavuni namba S 108648 D ilizimika ghafla katikati ya reli huku
kwa mbali wakiiona treni ya kutoka ubungo kwenda Stesheni katikati ya
jiji, maarufu kama ‘treni ya ‘Mwakyembe’ ikikaribia eneo walilokwama.
“Abiria
walikumbwa na taharuki huku wakiruka madirishani na wengine kugombea
kupita mlangoni kujinusuru kugongwa na treni,” alisema mmoja wa abiria
walionusurika.
Alisema
kilichowasaidia kutopatwa na maafa ni kitendo cha dereva kusimamisha
treni ili kupisha daladala hiyo kuondolewa katika njia yake.
Baadhi
ya abiria waliokuwamo kwenye daladala hiyo, walisema tangu wakitoka
Gongo la Mboto, ililonekana kuwa na matatizo na kwamba baada ya tukio
hilo, abiria walioruka kwenye daladala hilo hawakurejea tena kupanda kwa
kupatwa na hofu.
0 comments:
Post a Comment