Monday 18 December 2017

Antoine Griezmanna omba radhi mashabiki wake

Mchezaji wa klabu ya soka Atletico Madrid na timu ya Ufaransa, Antoine Griezmann, amelazimika kuomba radhi kufuatia kitendo chake cha kupiga picha akiwa amejipaka rangi nyeusi katika mwili wake na kisha kuituma katika mtandao wa kijamii akionekana kama mchezaji wa mpira wa kikapu.

Licha ya kuwa picha hiyo haikudumu muda mrefu tangu aitume, mamilioni ya wafuasi wa masuala ya michezo wameiona na kumshutumu kwamba anashiriki vitendo vya ubaguzi ambavyo ni haramu kwa wanamichezo

Lakini Griezmann mwenyewe, amejitetea kuwa, lengo kufanya hivyo ilikuwa ni kuonyesha kuwa yeye ni shabiki wa timu ya maonyesho ya mchezo mpira wa kikapu ya Harleem GlobeTrotters.

0 comments:

Post a Comment