Tuesday 26 December 2017

Mvua kubwa yaua watu 164 Ufilipino


Serikali ya Philippines imesema, watu 164 wamefariki na wengine 171 hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha kusini mwa nchi hiyo .
Mvua kubwa ilianza kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Mindanao ijumaa  na kusababisha mafuriko ya ghafla na maporomoko ya udongo katika eneo hilo. Watu elfu 98, wengi wakitoka familia za wakulima zenye hali duni ya kiuchumi, walisherehekea sikukuu ya Krismas katika vituo vya uokoaji vilivyowekwa na serikali.
Tume ya Kudhibiti Majanga nchini humo imesema, baadhi ya wakazi walipuuza wito wa serikali wa kuondoka kwenye maeneo yao kabla ya mvua hiyo kunyesha. Tume hiyo imesema barabara, madaraja, na mashamba yameharibiwa vibaya na mvua hiyo.

0 comments:

Post a Comment