Tuesday 26 December 2017

Rais Al- Sisi wa Misri azidi kukubalika


Misri ikielekea katika uchaguzi mkuu ndani ya timu inayomuunga mkono  rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri zimedai kuwa zimekusanya zaidi ya saini za wamisri milioni 12 wanaounga mkono Bw. Al-Sisi katika kugombea muhula wa pili wa urais katika uchaguzi utakaofanyika mwaka 2018.

Aidha  Bw. Al-Sisi mwenyewe hajatangaza kama atagombea urais au la, lakini anatarajiwa kupata ushindi mkubwa kutokana na kutokuwepo kwa mpinzani mwenye nguvu.
Kazi ya kukusanya saini hizo ilianza mwezi Septemba na kufanikiwa kuanzisha makao makuu 168 katika mikoa 27 nchini kote. 

Mratibu mkuu wa shughuli hiyo Bw. Mohamed al-Garhy amesema lengo kuu la shughuli hiyo ni kulinda Misri, akisisitiza kwamba rais Sisi anaweza kulinda nchi hiyo dhidi ya machafuko na mauaji kama yanayoonekana katika nchi nyingine za Kiarabu kama Syria , Libya na Yemen.

0 comments:

Post a Comment