Tuesday 26 December 2017

Timu ya Mbeya Kikapu yanyakuwa ushindi Taifa Cup



Timu ya mpira wa kikapu ya Mbeya imefanikiwa kutetea ubingwa wake msimu huu baada ya kuifunga timu ya mkoa wa Songwe katika mchezo wa fainali katika mashindano yaTaifa Cup yaliofanyika katika uwanja wa ndani jijini Dar es salaam.

Mbeya amabayo mpaka sasa imeshanyakua ubingwa mara  tatu mfululizo kwa timu hiyo ambayo kwenye mechi ya nusu fainali iliwafunga timu yenye historia ndefu ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa mbeya, Mboka Mwambusi, maandalizi pamoja na nidhamu za wachezaji ndiyo siri kubwa ya mafanikio ya timu hiyo katika misimu mitatu hii.

Ushindi wa pili katika Taifa Cup umekwenda kwa Songwe  ukifatiwa na  Dar es salaam kwa upande wa wanaume huku kwa upande wanawake ushindi umebaki kwa Dar es salaam,Mbeya(2nd)na Mjini Magharibi kutoka Zanzibar (3rd).
(MVP) Imekwenda kwa Musa Chacha(MBEYA) nafasi ya mkabaji bora imechukuliwa na Murshidi Mudricat(DSM) na katika naasi ya mfungaji bora imenyakuliwa na Baraka Sadick(SONGWE).

0 comments:

Post a Comment